Kudhamiria Kushinda

Kudhamiria Kushinda

Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, nyamaza utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. MARKO 4:39

Shukuru kuwa hakuna dhoruba maishani ambayo ni kubwa kuliko nguvu na makusudio ya Mungu. Unapokataa kuruhusu matatizo yako kukudhumu, basi hayatakukandamiza au kukufadhaisha. Ukimtazama Bwana, utasimama imara katika dhoruba na kuwasili salama mahali Mungu anapokusudia ufike.

Wakati wowote tunapojaribu kuchukua hatua na kumfanyia Mungu kitu, adui atakipinga. Bila shaka Paulo alishuhudia hili. Aliandika katika 1 Wakorintho 16:9: “Kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.”

Paulo alipingwa na wewe pia utapingwa. Ninakuhimiza kufanya uamuzi kwamba utafanya kile Mungu anakuambia ufanye. Usiwe na nia mbili, kutilia shaka uamuzi wako. Dhamiria kukaza mwendo na usikate tamaa. Amini Mungu, shukuru kwa nguvu zake, kaza mwendo hata iwe vipi.


Sala ya Shukrani

Asante, kwamba hakuna kilicho kigumu kwako. Nisaidie kukuegemea wakati kuna dhoruba inayopiga karibu nami. Ninakutazama leo, na ninakataa kudhulumiwa na shida yangu. Ninachagua kukustahi badala yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon