Badilisha Kufikiria Kwako kuhusu Hofu

Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako, nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. —ISAYA 41:10

Kwa usaidizi wa Mungu, unaweza kuondokwa kwa kutishika katika woga hadi kushinda woga kwa kubadilisha vile unavyowaza. Biblia inarejelea hili kama kufanya upya nia yako (Warumi 12:2). Kusema kwa urahisi, tunaweza kujifunza kuwaza kwa njia tofauti. Huenda tajriba au watu uliohusiana nao kitambo walikufundisha kuogopa, lakini Neno la Mungu linaweza kukufundisha kushinda woga huo. Unaweza kujifunza kuwa mjasiri, shupavu na mkakamavu.

Usiache woga wa kitu uzuie mafanikio na furaha yako katika kuishi kwako kwa kila siku. Woga una kivuli kikubwa, lakini woga wenyewe kwa kweli ni mdogo sana. Woga huleta mateso yasiyohitajika katika maisha yako. Unapohisi woga, si lazima ukate tamaa au urudi nyuma. Mungu yuko nawe, na kwa sababu yuko nawe, unaweza kuhisi huo woga lakini hata hivyo ufanye unalotaka kufanya.

Badala ya kufikiria huwezi kufanya kitu ukiwa na woga, fanya uamuzi kwamba utatimiza lengo lako na kushinda changamoto iliyo mbele yako. Huenda ukawa na mawazo ya woga, lakini Roho Mtakatifu ndani yako anaweza kubadilisha mawazo yako kuhusu woga. Woga huonekana kama jitu, lakini huwa linaondoka haraka linapokabiliwa na ukweli kutoka kwa Neno la Mungu. Woga ni kama watesaji wa skulini: hutesa kila mtu aliye karibu hadi mwishowe ajitokeze mmoja wa kulipa changamoto.


Tunapoogopa bado huwa tunateseka, bado huwa tunateseka kwa kitu tunachoogopa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon