Kufurahia Safari

Kufurahia Safari

Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu?… —Luka 10:40

Ninaamini kwamba maisha yanafaa kuwa sherehe. Waaminio wengi huwa hawafurahii maisha, acha tu hata kuyasherehekea. Kwa kweli watu wengi wanampenda Yesu Kristo na wako njiani kwenda mbinguni, lakini ni wachache tu wanaofurahia safari hiyo. Kwa muda wa miaka mingi, nilikuwa mmojawapo wa watu hao…Nilikuwa kama Martha!

Martha alikuwa akishughulika kufanya niliyokuwa nikifanya, kukimbia hapa na pale nikijaribu kufanya kila kitu kwa ukamilifu ili nimpendeze Mungu na kila mtu. Nilitatiza uhusiano wangu na Bwana kwa sababu nilikuwa na mtazamo wa kisheria kwa haki. Nilihisi tu vizuri kujihusu kila nilipotimiza kitu. Na nilichukia watu kama Mary ambao walifurahia maisha. Nilifikiri kwamba wangekuwa wanafanya kazi vile nilikuwa ninafanya.

Tatizo langu lilikuwa kwamba nilikuwa Martha na sio Mary. Nilimpenda Yesu, lakini sikuwa nimejifunza kuhusu maisha rahisi aliyotamani niishi. Jibu nililogundua lilikuwa na shina lake katika imani, kugundua maana ya kuketi miguuni pa Yesu, kusikiliza maneno yake, na kuamini Mungu kwa moyo na nafsi yangu yote.


Ukitaka kufurahia maisha, jifunze kuishi kwa usawa. Fanya kazi, abudu, cheza na upumzike. Kazi pasipo kufanya lolote, huzalisha mtu anayeishi maisha yaliyotatizika, changamano na yasiyo na furaha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon