Kugundua Kusudi Lako

Kugundua Kusudi Lako

Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele—usiziache kazi za mikono yako. ZABURI 138:8

Watu wengi wamechanganyikiwa kuhusu kile wanafaa kufanya na maisha yao. Hawajui mapenzi ya Mungu juu ya maisha yao; hawana mwelekeo. Iwapo hufanyi chochote na maisha yako kwa sababu huna hakika unataka kufanya nini, basi ninapendekeza uombe, shukuru Mungu kwamba ana kusudi kwa ajili yako, na uanze kujaribu kufanya vitu vingine. Haitakuchukua muda mrefu kabla hujaanza kuhisi unapenda kitu fulani. Kitakuwa sawa kabisa kwako.

Fikiria hilo hivi: unapoenda kununua nguo mpya, bila shaka huwa unajaribu nguo nyingi hadi upate inayokutosha vizuri, inayofaa na inayoonekana vizuri kwako. Kwa nini usijaribu kitu kama hicho katika jitihada za kugundua kusudi lako? Tunapochukua hatua ya imani, kusudi letu linafunuliwa. Mtu mwenye shukrani hujua Mungu yuko naye. Haogopi kufanya makosa, na akiyafanya, anapata nafuu na kuchuchumilia mbele.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kuwa una kusudi la kiungu kwa ajili ya maisha yangu. Ninapotoka nje kwa imani, nisaidie kutambua mpango wako mwema kwa ajili ya mustakabali wangu. Ninashukuru kuwa unatembea nami ninapotafuta kutembea katika njia zako maishani mwangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon