Kujazwa na Roho Mtakatifu

Basi, ikiwa ninyi mlio mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? —LUKA 11:13

Tunahitaji kujazwa Roho Mtakatifu sisi wote bila kikomo. Kama waaminio ndani ya Yesu, tuna Roho Mtakatifu, lakini pengine hatujajisalimisha kabisa kwake kwa matumizi yake. Hivyo ndivyo ilivyotendeka kwangu kwa miaka mingi hadi nikafika mahali pa hatari katika maisha yangu ambapo sikuhiari kuchechemea siku baada ya nyingine bila ushindi wa kweli.

Nilimwomba Mungu afanye “kitu,” na nilikuwa tayari kwa mpango wowote ule aliokuwa nao! Hata sikujua nilichohitaji, lakini Mungu alijua. Yeye huwa mwaminifu wakati wote kukutana nasi mahali tulipo na kutusaidia kufika tunakohitaji kuwa.

Nilihitaji kujazwa Roho wa Mungu, na kwa neema zake na rehema, nilijazwa. Bado huwa ninamwomba Mungu kila mara kunijaza upya na uwepo wake na nguvu na kuniwezesha kuwa kila kitu anachotaka niwe. Tunahitaji nguvu za Roho Mtakatifu ili tutende mapenzi ya Mungu. Usiwahi kujitegemea, kwa kuwa mbali naye, huwezi chochote (Yohana 15:5).

Omba ujazo mtimilifu wa Roho wa Mungu kila siku na utakuwa na uzoefu wa kuwa karibu na Mungu ambao ni wa ajabu. Roho Mtakatifu anapokuja juu yako, basi unapokea nguvu za kuwa shahidi wake. Utabadilika kwa njia za ajabu unapotumainia nguvu za Mungu kukuwezesha na kukutia nguvu.


Omba na upokee nguvu za Roho Mtakatifu katika maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon