Kukubaliana na Mungu

Kukubaliana na Mungu

Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi. 1 TIMOTHEO 6:12

Chukua hatua ya imani na bila kujali vile unavyohisi, kubaliana na Mungu kuwa anakupenda. Umeumbwa kwa njia ya ajabu na una vipawa vingi na nguvu. Wewe ni wa maana, na kama mwaminiye ndani ya Yesu, wewe ni mwenye haki wa Mungu ndani yake. Una haki mbele ya Mungu badala ya dhambi—shukuru kwa kipawa hicho cha ajabu!

Anza kuongea kinyume na hisia za kukosa usalama na useme, “Mimi ni wa Mungu na ananipenda!” (tazama Waefeso 2:10). Tunaamini mengi ambayo tunajisikia tukisema kuliko yale ambayo wengine wanasema, kwa hivyo anza kusema kitu fulani kizuri na uzamishe sauti zingine zinazokuhukumu.

Jipiganie! Pigana vita vizuri vya imani na ukatae kuishi chini ya kiwango ambacho Yesu anataka uishi. Ufalme wake ni haki, amani na furaha (tazama Warumi 14:17). Usikubali kingine kidogo kuliko hicho.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba ninaweza kutangaza kwa imani mimi ni nani ndani ya Yesu. Ninashukuru kwa kuwa uliniumba kwa njia maalum na unanipenda sana. Leo ninachagua kuamini kwamba mimi ni kazi ya mikono yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon