Kumngoja Bwana

Kumngoja Bwana

Nafsi zetu zinamngoja Bwana; yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu. —ZABURI 33:20

Katika jamii yetu ya pupa na kutaka vitu vifanyike haraka, nidhamu ya kiroho ya kumngoja Bwana hukosekana. Tunataka kila kitu tunachotaka na tunakitaka sasa hivi! Lakini tukiwa katika haraka kama hizo wakati wote, tutakosa ushirika wa karibu na Mungu ambao huchukua muda kukua. Mungu anataka kuzungumza na mioyo yetu iwapo tu tutakuwa na subira ya kusikiliza.

Eliya alikuwa mtu aliyejua siri ya kuwa na subira. Baada ya kuwaua manabii wa Baali, Eliya alijifunza funzo la thamani kuhusu kumngoja Mungu. Bwana alimwambia Eliya atoke asimame mlimani na angoje. Upepo mkuu ukaja; halafu kukaja tetemeko kuu la nchi na moto mkuu, lakini Bwana hakuwemo katika vitu hivyo. Fikiria vile 1 Wafalme 19:12 inasema: “Na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.” Bwana alizungumza kwa sauti tulivu ndogo, baada ya upepo, tetemeko la nchi, na moto. Eliya asingekuwa na subira katika maombi, asingesikia sauti ya Mungu.

Daudi alijifunza pia kungoja katika nyumba ya Bwana na “kutafakari, kufikiria na kumwuliza mambo (Zaburi 27:4). Ili tuombe kwa mafanikio, tunaweza kuchagua kungoja kwa subira na kusikiliza Neno kutoka kwake. Kungoja na kusikiliza hutoa fikra juu yetu na kuziweka juu yake, ambaye ni jibu la mahitaji yetu yote.


Mara nyingi ni katika utulivu ambapo nguvu za Mungu hufanya kazi kwa njia kuu. Ruhusu Roho Mtakatifu kukufundisha jinsi ya kungoja katika uwepo wake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon