Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina! Warumi 11:36
Kila kitu Mungu hutuambia tufanye ni kwa ajili ya mema yetu. Maagizo yake yote kwetu yanakusudiwa kutuonyesha njia ya kuelekea kwenye haki, amani na furaha.
Yesu hakufa kwa ajili yetu ili tuwe na dini, lakini ili tuwe na uhusiano wa kibinafsi na Mungu ulio wa karibu na wa ndani kupitia kwake. Anataka tuishi naye, kupitia kwake na kwa ajili yake. Alituumba kwa ajili ya ushirika—hicho ni kitu cha kushukuru kwacho! Kitu ambacho watu wengi wanakosa kutambua ni kwamba hawawezi kutimilika au kuwa na ridhaa wanayotamani bila Mungu. Alituumba kwa sababu ya raha na furaha yake. Hutupatia uzima kama kipaji, na kama tutamregeshea bila kushurutishwa, basi ni wakati huo tu tutakaouishi kitimilifu kwa furaha tele.
Sala ya shukrani
Ninakushukuru leo, Baba, kwa kipaji cha uhusiano nawe kupitia kwa Kristo Yesu. Ninashukuru sana kwamba kila kitu unachoniambia kufanya ni kwa ajili ya manufaa na mema yangu. Asante kwa kuwa una mpango wa ajabu juu ya maisha yangu.