Kumtumainia Mungu

Kumtumainia Mungu

Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana Mungu, tumaini langu tokea ujana wangu. ZABURI 71:5

Kuamini Mungu huturuhusu kuingia katika utulivu wake, na utulivu ni mahali pa amani ambapo tunaweza kufurahia maisha huku tukiwa na hakika kwamba Mungu atapigana vita vyetu.

Mungu hutujali sisi wote; atasuluhisha matatizo yetu na kutimiza mahitaji yetu, na kwa shukrani tunaweza kukoma kuwaza na kuwa na wasiwasi kuyahusu. Ninatambua hili ni rahisi kusema kuliko kutenda, lakini hakuna muda mwingine kama wa sasa ambao tunaweza kuanza kujifunza njia mpya ya kuishi njia ya kuishi ambayo haina wasiwasi, mfadhaiko na hofu.

Huu ndio wakati wa kuanza kuamini na kusema, “Ninaamini Mungu kikamilifu; hakuna haja ya wasiwasi! Sitakubali hofu au wasiwasi. Mungu ni chanzo cha imani yangu.” Kadri unavyofikiri kuhusu ukweli huu, ndivyo unavyojipata ukichagua imani juu ya wasiwasi.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwamba si lazima niwe na wasiwasi ! Ninaamini huwa unanijali na kuwa nami kila wakati.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon