Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; ni tamu nafsini, na afya mifupani. —MITHALI 16:24
Sehemu muhimu ya kujifunza kupenda watu wengine ni kuwapenda kwa maneno yetu. Nguvu na himizo tunalowapa kwa maneno yetu huleta tofauti! Watu kila mahali huhitaji watu wanaowaamini. Wamedhuriwa kwa maneno mabaya, lakini maneno mazuri yanaweza kuleta uponyaji katika maisha yao.
Ni rahisi kuonyesha udhaifu, upungufu na makosa ya wale wanaotuzunguka. Hili ni jambo la kawaida linalotoka katika mwili wetu. Lakini haya maneno hayaleti uzima—yanakuza yote yaliyo mabaya kuhusu watu na hali. Lakini Biblia inasema katika Warumi 12:21 kwamba tuushinde ubaya kwa wema.
Kadri tunavyomkaribia Mungu, ndivyo tunavyojifunza kuzungumza maneno mazuri ya uzima yanayotia nguvu. Mungu ana mawazo mema na tunapotembea naye, tutajifunza kukubaliana naye (Amosi 3:3).
Ni rahisi kupata makosa kwa kila mtu, lakini upendo hauzingatii makosa ya wengine. Petro wa kwanza 4:8 inasema hivi: “Zaidi ya yote, iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi [husamehe na kupuuza makosa ya wengine].”
Kuamini mazuri kuhusu watu na kunena maneno yanayowajenga ni njia muhimu ya kuwapenda.