Kuomba ombi la “Sasa Hivi”

Kuomba ombi la “Sasa Hivi”

Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 1 YOHANA 5:14

Mara nyingi huwa tunasikia kuhusu hitaji la maombi au kufikiria kuhusu hali na kujiambia, ninahitaji kuomba kuhusu hilo baadaye nitakapokuwa nikiomba. Hilo wazo ni mbinu ya kukwamisha ya adui. Kwa nini usiombe dakika hiyo hiyo? Uhairishaji ni mojawapo ya vitu vikuu ambavyo shetani hutumia kutuzuia ili tusiwahi kufanya kitu kizuri. Usiwahi kusitisha hadi baadaye kile unachoweza kufanya sasa hivi!
Maombi yatakuwa rahisi iwapo tutafuata mioyo yetu, lakini shetani anataka uhairishe kwa sababu anatumaini kwamba tutasahau jambo hilo kabisa.

Moyo wenye shukrani tayari umemlenga Bwana na uko tayari kuomba wakati wowote. Kuomba tunapohisi tamaa au hitaji la kuomba ni rahisi kufanya, na ndio vile tunavyoweza kuomba bila kukoma na kubaki tukiwa tumeunganishwa na Mungu katika kila hali mchana wote.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwa nguvu za maombi. Hitaji la maombi ninalohitaji kushughulikia likinijia, nitaongea nawe kulihusu mara moja. Asante kwamba wewe huwa tayari kusikiliza maombi yangu wakati wote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon