Kushikilia Tumaini

Kushikilia Tumaini

Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana? Matumaini yangu ni kwako. ZABURI 39:7

Neno la Mungu linasema kwamba anataka tubarikiwe (tazama Kumbukumbu la Torati 29:9). Inasema kuwa tunaweza na tutabaririkiwa kwa kila njia tukitembea katika mapenzi ya Mungu. Shetani anataka watu waishi kwa woga, bila tumaini. Kukosa tumaini huiba amani na furaha yetu tuliyopewa na Mungu.

Adui huwaambia watu hawatawahi kuwa na kitu, maisha yao hayatawahi kubadilika, na mambo hayatawahi kuwa mazuri. Na watu wakiamini uongo wake, wanakaa bila tumaini na kukata tamaa. Tunapokea tunachoamini, kiwe chanya au hasi, kwa hivyo ni muhimu kwetu kuwa na imani ndani ya Mungu bila kukoma, vile Marko 11:22–24 inavyotuambia kufanya.

Kataa kuwa mwenye kukosa tumaini na utie imani yako ndani ya Neno la Mungu. Kuwa kama Ibrahimu, ambaye inasemekana kwamba ingawa hakuwa na sababu ya kutumaini, alitumaini kwa imani kwamba ahadi za Mungu zitatimia katika maisha yake. Aliposubiri, alitoa sifa na utukufu kwa Mungu, na Shetani hakuweza kumshinda kwa shaka na kutoamini (tazama Warumi 4:18–20).


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa nguvu za tumaini. Ninashukuru kwamba bila kujali hali zinazonizunguka, ninaweza kuweka imani yangu ndani yako na katika Neno lako. Nina amani leo kwa sababu wewe ndiwe chanzo cha tumaini langu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon