
Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo. 2 WAKORINTHO 10:5
Shetani ametangaza vita dhidi ya watoto wa Mungu, na nia zetu ndizo uwanja wa vita ambamo ushindi au ushinde wa vita hivyo hufanyika. Shetani anapenda kutia mawazo mabaya katika nia zetu—mawazo ambayo hayakubaliani na Neno la Mungu—akitumai kwamba tutayatafakari kwa muda mrefu unaotosha ili yafanyike katika maisha yetu. Tunaweza kuyaangusha hayo mawazo yasiyo mazuri na kuyateka nyara ili yaweze kumtii Yesu Kristo.
Shukuru kwamba unaweza kuchagua mawazo yako binafsi na kwamba wewe si mfungwa wa aina yoyote ile ya mawazo inayoanguka katika nia yako. Fikiria kimaksudi vitu vizuri vinavyokubaliana na Neno la Mungu. Fikiria kuhusu upendo wa Mungu kwako na mpango mzuri alio nao juu ya maisha yako. Fikiria kuhusu vile unavyoweza kuwa baraka kwa watu wengine na vile unavyoweza kuwa baraka kwa Mungu kwa kupatikana tu naye kwa urahisi ili afanye kazi kupitia kwako. Kufikiria fikra nzuri kutafunga mlango kwa fikra mbaya, na katika mchakato huo, mlango unafungika kwa shetani pia.
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru Baba, kwamba mimi ni mwanao na nimebarikiwa sana. Leo, ninachagua kufikiri fikra zinazomtukuza Mungu, nikilenga wema wako katika maisha yangu. Ninashukuru kwamba ninaweza kuchagua fikra ambazo nitakazolenga kufikiri.