Kushindwa au Tukio la Kuleta Mafanikio?

Kushindwa au Tukio la Kuleta Mafanikio?

Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidi wampendao. YAKOBO 1:12

Hakuna anayejitayarisha kushindwa au kutaka kushindwa. Lakini “kushindwa” kunaweza kuwa tukio la kuleta mafanikio katika njia ya kuelekea kwenye ufanisi. Kwa hakika kushindwa hutufundisha kile hatufai! Kufanya kushindwa kuwe chanya inategemea vile tunavyoona kushindwa huko. Tunaweza kujifunza kushukuru kwa ajili ya kushindwa kwetu.

Hadithi nyingi zimezunguka kuhusu vile Thomas Edison alishindwa mara nyingi kabla aasisi balbu ya nuru. Nimesikia kwamba alijaribu mara 700, mara 2,000, mara 6,000 halafu mara 10,000. Hata kama alifanya mara ngapi, idadi hiyo ni ya kushangaza. Lakini hakukata tamaa. Edison anaripotiwa kusema kwamba katika jitihada zake zote, hakuwahi kushindwa—si hata mara moja; alilazimika tu kupitia hatua nyingi sana ili kupata mambo sahihi! Inachukua aina hiyo ya uamuzi iwapo utafanya kitu chochote cha maana.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba unaweza kuchukua hata kushindwa katika maisha yangu na kuutumia kufanya kitu cha ajabu. Ninaamini kwa imani kwamba unafanya kitu cha nguvu katika maisha yangu. Ninakushukuru mapema kwa yale ninayojifunza, hata katika nyakati ngumu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon