wasiwasi ni ubinafsi uliojificha

wasiwasi ni ubinafsi uliojificha

Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi. Warumi 14:23

Mara nyingi, watu wanajikuta na wasiwasi bila kutambua jinsi ilivyo na uharibifu mkuu. Unapotazama kwenye mizizi yake, wasiwasi ni dhambi. Hakika haitokei kwa imani, na Warumi 14:23 inasema kwamba Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.

Mara nyingi, wasiwasi hutegemea dhambi moja hasa: ubinafsi. Kawaida tunapokuwa na wasiwasi, tuna wasiwasi juu ya jinsi tamaa zetu za ubinafsi hazikutimizwa. Zaidi unavyokuwa na tamaa za ubinafsi ndivyo unavyozidi kuwa na wasiwasi kuzihusu, na ndivyo maisha yako yanakuwa magumu.

Mungu anataka sisi tuzingatie kumtumikia.

Ni mapenzi ya Mungu kwamba tuishi maisha yetu bila ya wasiwasi yoyote na hofu isiyofaa. Anataka tuwe huru kumtumikia bila kuchanganyikiwa (tazama 1 Wakorintho 7:34).Hatupaswi kuruhusu wasiwasi ya ulimwengu huu kutugeuza kutoka kwa kusudi lake kwa maisha yetu.

Muombe Mungu akusaidie kutambua na kujiondolea tamaa za ubinafsi. Hii itaweka maisha yako rahisi na kukusaidia kushinda wasiwasi. Kisha unaweza kutekeleza kwa moyo wote mpango mkuu wa Mungu kwa maisha yako.

OMBI LA KUANZA SIKU

Baba Mungu, asante kwa kunionyesha kuwa wasiwasi ni dhambi. Nisaidie kuondokana na tamaa zangu za ubinafsi, zilizo na uchafu ili nipate kufuata hatima yako kwa ajili yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon