Kusubiri Upenyo

Kusubiri Upenyo

Daudi akasema, Bwana amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu. 1 MAMBO YA NYAKATI 14:11

Kuna nyakati nyingi ambazo watu hukata tamaa kabla tu ya upenyo—kwenye ukingo wa ushindi haswa. Lakini usikate tamaa! Unaweza kusubiri kwa miaka kumi halafu mara tu, siku moja unaamka na kila kitu kimebadilika. Ndoto yako hatimaye imetimizwa, hali ambamo uliishi kwa muda mrefu imeisha, au mwishowe ulipata kitu ulichofanyia kazi kwa muda mrefu.

Shukuru kwamba Mungu ana mpango juu yako na amesikia maombi yako—huenda usitambue vile ulivyo karibu sana na upenyo wako. Hata kama itakulazimu kusubiri miaka mitatu, minne, mitano au zaidi, iwapo utaendelea kuukaza mwendo, kwa shukrani utakuwa na ushindi unaohitaji. Chochote unachofanya, usikate tamaa, usikate tamaa kwenye ukingo wa upenyo wako. Usiache kutumaini, kuamini, na kumtii Mungu. Badala yake sema, “nitaendelea; sitawahi kukata tamaa.”


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba upenyo wangu uko njiani. Nina tumaini na siko peke yangu. Uko nami, na una mpango mwema juu ya maisha yangu. Ninakuamini Bwana na ninakataa kukata tamaa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon