Kutoa na Kupokea Upendo

Kutoa na Kupokea Upendo

Amri mpya nawapa, mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo vivyo. YOHANA 13:34

Miongoni mwa vitu vyote ambavyo tunastahili kutolea shukrani katika maisha yetu, upendo ndio wa kwanza katika orodha. Kupenda na kupendwa huleta kusudi na maana kwa maisha. Ulimwengu unatafuta upendo, lakini kwa kweli wanatafuta Mungu kwa sababu Mungu ni upendo.

Watu hutafuta utimilifu maishani kwa njia nyingi ambazo huenda zikaonekana kuwa nzuri mara ya kwanza lakini huwaacha wakihisi kukata tamaa na kusikitika, na utupu. Ni kwa kupokea tu upendo wa Mungu na kutembea kwa upendo (kuonyesha upendo kwa matendo kwa kuendelea kufikia wengine na kujaribu kuwaonyesha upendo kupitia kwa vitendo mbalimbali vya ukarimu) ndipo wanaweza kupata utimilifu wa kweli wa Mungu ambao wanatafuta kwa bidii.

Upendo utabadilisha maisha yako! Muombe Mungu akusaidie kupokea na kupeana upendo, na kuwa mwenye shukrani unapotazama upendo wake ukileta utimilifu ambao hujawahi kujua katika maisha yako.


Sala ya Shukrani

Baba, nimejawa na shukrani kwa kuwa unanipenda na kwamba umenipa uwezo wa kuwapenda wengine. Acha upendo wako utiririke kupitia kwangu leo kwa njia ambazo zitakuwa baraka kwa wengine.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon