Kuvaa zawadi ya haki ya Mungu

 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye. 2 Wakorintho 5:21

 Hapa kuna maswali mawili muhimu sana unayohitaji kujiuliza:

Je, ninajua mimi ni nani katika Kristo?

Je, ninaenenda kwa haki?

Watu wengi hawawezi kujibu maswali haya vizuri, na hii huwazuia wasiishi katika uhuru na amani ambayo Mungu alikusudia kwao kuingia. Wakati tunapompokea Yesu Kristo kama Mwokozi wetu, Biblia inasema Mungu anaondoa dhambi zetu na anatupa haki yake. Ni zawadi, ambayo hatuna haja ya kuigharamia. Lakini tunahitaji kuivaa. Na kila wakati tunapofanya hivyo, tunapokea amani Yake. Unapojua wewe ni nani ndani ya Kristo, unakuwa na amani na ujasiri kwamba Mungu atakupa kila unachohitaji kufanya kile unachohitaji kufanya. Unapojua kwamba anakupenda na alikufa kwa ajili yako, unaweza kuamka kila siku na kufanya kadri uwezavyo kumpenda Mungu.

Na unapojua wewe ni nani ndani ya Kristo, unaweza kuvaa na kutembea katika haki ambayo alikununulia. Unapopata upendo wake kwa ajili yako, jibu lako la kawaida litakuwa kwa ajili yake kwa kila kitu ulicho nacho.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, nataka daima kujua mimi ni nani ndani yako. Nisaidie kukumbuka yote uliyonifanyia ili nipate kuvaa haki yako kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon