Jiweke kwenye sahani ya sadaka

Jiweke kwenye sahani ya sadaka

Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Warumi 12:1

Katika 2 Wakorintho 8, Paulo alipozungumza na waumini wa Korintho kuhusu kutoa, aliwapa mfano wa makanisa huko Makedonia. Alisema katika mstari wa 5, Wala [haikuwa ni zawadi yao tu mchango] tulivyotarajia, lakini kwanza walijitoa kwa Bwana na kwetu [kama wajumbe Wake] kwa mapenzi ya Mungu [wasijali kabisa maslahi yao, wao walitoa kwa kadiri walivyoweza, baada ya kujiweka wenyewe kwa kuongozwa na mapenzi ya Mungu].

Hiyo inanishangaza, kwa sababu hawakuwapa fedha zao tu – bali walijitoa wenyewe.

Nashangaa ni wangapi wetu walio tayari kuandika majina yetu chini ya sahani ya sadaka. Warumi 12: 1 inasema tunapaswa kujitoa sisi wenyewe kama sadaka kwa Mungu.

Hii inamaanisha kuishi kwa Mungu nje ya kanisa. Ina maana kuwa nia ya kutoa fedha, lakini pia inamaanisha kuwa tayari kumpenda mtu yeyote ambaye Mungu huleta kwenye njia yako. Ina maana kuwa tayari kutumia rasilimali yoyote uliyo nayo kwa ufalme Wake.

Kwa hiyo wakati mwingine utakapokuwa kanisani na sahani ya sadaka ije karibu, nakuhimiza kumwambia Mungu kwamba unajitoa kwake mwenyewe!

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nataka kutoa yote niliyo nayo. Ninajitoa mwenyewe kama sadaka hai. Nionyeshe jinsi unataka mimi kutumia rasilimali uliyonipa kwa utukufu wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon