Kuwa Jasiri Kila Wakati

Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, mwenye haki ataishi kwa imani. — WARUMI 1:17

Ujasiri una shina katika imani ndani ya Mungu. Hii ndiyo kwa sababu ni muhimu kwamba tuchague jasiri kila wakati sio jasiri mara moja moja.

Nililazimika kuendelea kuwa jasiri nilipoambiwa na marafiki pamoja na familia kwamba mwanamke hafai kuwa akifundisha Neno la Mungu. Nilijua Mungu alikuwa ameniita kufundisha Neno la Mungu, lakini nilikuwa nimeathiriwa na kukataliwa na watu bado. Ilibidi nikue katika ujasiri hadi mahali ambapo maoni ya watu, kunikubali au kunikataa kwao kuliacha kuathiri kiwango cha ujasiri wangu. Ilibidi ujasiri wangu uwe ndani ya Mungu wala sio watu.

Warumi 1:17 inasema kwamba, tunaweza kwenda kutoka imani hadi nyingine. Niliishi miaka mingi nikienda kutoka imani hadi shaka kisha kwenye kutoamini hadi kwa imani. Kisha nikatambua kwamba nikipoteza ujasiri wangu, ninamwachia shetani mlango uliofunguka. Nikimruhusu kuiba ujasiri wangu, nitakosa imani ya kuhubiria watu ghafla.

Ukitaka kufaulu, chagua kuwa jasiri kila mara. Kuwa jasiri kuhusu vipawa vyako, na mwito, uwezo wako ndani ya Yesu. Amini kwamba unasikia kutoka kwa Mungu na kwamba unaongozwa na Roho Mtakatifu. Kuwa jasiri ndani ya Bwana. Jione kama mshindi ndani yake.


Kujua upendo mkuu wa Mungu juu yako hukufanya kuwa na ujasiri mkuu wa kufanya mambo makubwa!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon