. . . Ndugu sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele, nakaza mwendo, nifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. —WAFILIPI 3:13–14
Kujuta kuhusu yaliyopita ni mwizi mkuu wa furaha na amani. Hata kama makosa yalifanywa miaka ishirini iliyopita au dakiki ishirini zilizopita, hakuna unaloweza kufanya kuhusu hilo isipokuwa kutubu, kupokea msamaha, kusahau yaliyopita na kuendelea. Kama kuna kitu unchoweza kufanya kufumua matokeo ya makosa yako, basi kwa hali yoyote, fanya hivyo. Lakini la muhimu ni kwamba lazima uachilie yaliyopita ili ushikilie siku zijazo.
Kama Paulo, tunachuchumilia mbele kwenye utimilifu, lakini hakuna mmoja wetu aliyewasili. Hata ingawa alivumilia matatizo, ninaamini Paulo alifurahia safari ya maisha na huduma yake, na hilo “tamanio lake moja” ndilo lilikuwa mojawapo ya sababu. Alikuwa amejifunza kusahau makosa yake na kukataa kuishi katika majuto ya mambo yaliyopita.
Kila mara kumbuka kwamba majuto huiba sasa! Mungu ametuita kuwa karibu naye katika sasa. Tukishikilia yaliyopita, tunaweka kando imani na kuacha kuamini, halafu tunapoteza amani na furaha yetu.
Acha siku hii iwe ya uamuzi kwako—siku ambayo unaamua kwamba hutaendesha maisha yako katika majuto. Kuwa mtu wa sasa. Ishi katika wakati uliopo. Mungu ana mpango juu yako sasa. Mtumainie leo.
Mungu hutoa neema, furaha, na amani ya leo, lakini hatoi neema ya jana kwa sababu ya leo au kesho. Ishi siku moja kwa wakati mmoja.