Kuwa na mwanzo mpya

Kuwa na mwanzo mpya

na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; Waefeso 4:23

Biblia imejaa hadithi kuhusu watu ambao walipata mwanzo mpya. Musa akawa kiongozi baada ya kuwa mchungaji kwa miaka arobaini. Paulo alimchukia Kristo mpaka Mungu alipomfanya upya na kumfanya awe mmoja wa mitume wakuu wa wakati wote.

Tunapompokea Yesu kama Mwokozi wetu, ni mwanzo mpya kabisa. Tunakuwa viumbe vipya wenye fursa ya kujifunza njia mpya ya kuishi. Lakini hatua ya kwanza ya kupata maisha mapya hayo ni kuamini kuwa inapatikana kwako.

Waefeso 4:23 inasema tunapaswa kuwa daima upya katika mawazo yetu na mitazamo. Ni rahisi kusoma kuhusu watu wazuri katika Biblia na kufikiri kuwa wewe si kitu kama wao, lakini unapoanza kufikiri hayo, unahitaji kuifanya upya akili yako mara moja. Chagua kufikiri kulingana na Neno la Mungu-sio jinsi unavyohisi. Pata upendo wake na ujifunze mwanzo mpya.

Maisha yatakuwa matamu sana ikiwa unaishi na mtazamo unaosema, Mungu ananibadilisha kabisa kutoka ndani. Ananipa mwanzo mpya na kuna mambo makubwa zaidi mbele yangu.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, nataka kurekebisha mawazo yangu kupitia Neno lako. Najua kwamba una mwanzo mpya na wito kwangu kama vile ulivyofanya kwa Musa na Paulo. Ninaipokea leo, naamini kwamba Unaweza kuyatimiza.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon