
Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako, daima, naam, hata milele. ZABURI 119:112
Kama vile Biblia inavyotufundisha kumsifu Mungu na kumwabudu, inatupatia pia sababu za kumshukuru na kutufundisha jinsi ya kutoa shukrani zetu kwake, vile inavyoonyeshwa katika Maandiko yafuatayo:
- Ee Mungu, twashukuru. Twashukuru kwa kuwa Jina lako li karibu; watu huyasimulia matendo yako ya ajabu. Zaburi 75:1
- Ni neno jema kumshukuru Bwana, na kuliimbia jina lako, ee Uliye juu. Zaburi 92:1
- Tuje mbele zake kwa shukrani, tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Zaburi 95:2
- Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru, nyuani mwake kwa kusifu; mshukuruni, lihimidini jina lake Zaburi 100:4
Sala ya Shukrani
Baba, ninashukuru kwa ahadi na mafunzo ninayopata katika Neno lako. Leo ninachagua kuishi maisha ya shukrani kwa sababu unanifundisha Neno la Mungu. Nitakuwa mtiifu na ninaamini kwamba Neno lako hunifundisha njia bora zaidi ya kuishi.