Neno la Mungu ni dawa nzuri

Neno la Mungu ni dawa nzuri

Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. Zaburi 107:20

Wengi hufanya kosa la kubadili imani katika uponyaji kwa kuchukua dawa ya Mungu-Neno Lake. Wanasema, “Ninaamini katika uponyaji,” bila kutumia au kulinena Neno. Je! Dawa inaweza kufanya nini kwetu ikiwa hatutaichukua?

Neno la Mungu ni dawa yake-ni wakala wa uponyaji, kama vile dawa ya asili ni wakala wa uponyaji au kichocheo. Kwa maneno mengine, dawa yenyewe ina uwezo wa kuleta uponyaji. Ndani ya Neno la Mungu ni uwezo, maisha, nguvu ,na asili ya kuleta uponyaji kwa mwili wako.

Kwa hiyo tunachukuaje? Ni kama Neno la Mungu linapokua na mizizi moyoni mwako na linakaa pale ili lizalishe uponyaji katika mwili wako. Akili na ujuzi pekee hautafanya hivyo. Maandiko yanapaswa kuingia ndani ya akili na moyo wako kwa kutafakari-kuisoma, kuisikia, kutafakari na kuyazungusha kote kote katika akili yako – ili kuzalisha uponyaji katika mwili wako. Na wakati ule Neno limeingia ndani ya moyo wako, linaweza kuleta afya kwa mwili wako wote. Hebu Neno la Mungu liende ndani ya moyo wako leo

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, ninachagua leo kutafakari juu ya Neno lako la uponyaji. Kwa Neno lako ndani ya moyo wangu, najua uponyaji wako utajaza mwili wangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon