Kwa kuwa mimi Bwana sina kigeugeu ndio maana ninyi hamkuangamizwa enyi wana wa Yakobo. MALAKI 3:6
Kila kitu hubadilika isipokuwa Mungu—tunaweza kushukuru kwamba yeye ndiye aliye thabiti, chanzo kisichobadilika cha maisha yetu. Kuruhusu mabadiliko yote yanayofanyika karibu nasi kutufanya tufadhaike haitafanya mabadiliko yasiendelee kufanyika. Watu hubadilika, hali hubadilika, miili yetu hubadilika, matamanio na hisia zetu hubadilika. Kitu kimoja cha hakika katika ulimwengu huu ni mabadiliko.
Mabadiliko mengi hufanyika bila ruhusa yetu. Lakini shukuru, kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu, tunaweza kuchagua kubadilika pia. Tukikataa kufanya mabadiliko hayo katika mawazo na nia zetu, basi tunafanya makosa makubwa. Kukataa kwetu kubadilika hakubadilishi hali, lakini huiba amani na furaha yetu. Kumbuka, kama huwezi kufanya lolote kuhusu hilo, mtwike Bwana fadhaa zako (tazama 1 Petro 5:7) na uamini kwamba atakushughulikia.
Sala ya Shukrani
Ninashukuru, Baba, kwamba wakati kila kitu karibu nami kinaonekana kubadilika na kukosa uhakika, ninaweza kuamini kwamba hutawahi kubadilika. Nisaidie kukutazama wewe badala ya hali yangu. Ninakushukuru kwamba wewe ni msingi wa maisha yangu.