Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Mathayo 16:26
Mafanikio na thamani yetu ya kweli katika maisha haipatikani katika kile ulimwengu unafikiri ndiyo ngazi ya mafanikio. Sio katika kupandishwa cheo kazini, nyumba kubwa, gari zuri, au kuwa katika ushirika wa watu wanaoweza kukusaidia. Shukuru kwamba mafanikio ya kweli ni rahisi kuliko mambo hayo…na yenye nguvu zaidi.
Mafanikio ya kweli ni kumjua Mungu na nguvu za ufufuo wake. Ni kujua kwamba anakupenda bila masharti na kuwa umekubalika ndani ya Yesu, Mwana Mpendwa wa Mungu, aliyekufa kwa ajili yako kulipia dhambi zako. Mafanikio ya kweli yanapatikana katika kumwishia Mungu na utukufu wake. Kuwa msimamizi mzuri wa uwezo na rasilmali ambazo Mungu amekupa na utakuwa na hakika ya kufanikiwa, kwa sababu yuko nawe katika kila hatua njiani.
Usiwahi kujilinganisha na mtu mwingine yeyote kukadiria iwapo umefanikiwa. Kuwa aina nzuri sana yako ambayo unaweza kuwa. Wewe ni mafanikio!
Sala ya Shukrani
Baba, asante kwa kuwa mafanikio ya kweli yanapatikana ndani yako na sio katika kitu chochote ambacho ulimwengu unaweza kupeana. Ninashukuru kwamba nina kipaji cha wokovu na kwamba uko nami wakati wote. Ninapofanya mazuri kwa ajili yako, ninajua kwamba ninakusudiwa kufanikiwa.