Mungu Hukimu Mahitaji Yako kwa Wingi

Mungu Hukimu Mahitaji Yako kwa Wingi

Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire kama watu wasemavyo hata leo, katika mlima wa Bwana itapatikana. MWANZO 22:14

Ni muhimu kujenga nia ya wingi—ile ambayo inaamini Mungu atatoa kile tunachohitaji na kushukuru mapema kwamba atafanya hivyo.
Kote kwenye maandishi, Mungu anaahidi kuwapa wanawe. Kwa kweli, katika Agano la Kale, mojawapo ya majina ya Kiebrania ya Mungu ni “Yehova-yire,” ambayo inamaanisha Bwana Mpaji Wetu. Mimi na wewe ni wana wa Mungu. Yeye ni Baba yetu, na hufurahia kutupatia vile tu wazazi wetu wa mwilini hufurahia kusaidia watoto wao.

Kwa udhahiri, kila rasilmali ya mbingu na dunia iko mikononi mwa Baba, kwa hivyo hakuna kitu tunachohitaji ambacho hawezi kutupatia. Kwa kweli hakuna mtu ambaye anaweza kugawa baraka zake isipokuwa wanawe. Anza kumshukuru Mungu kwamba kila kitu unachohitaji chaja kwako sasa hivi!


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru sana kwamba wewe ni Yehova-yire. Bila kujali ninavyohisi au vile hali yangu ilivyo, nitakutazama wewe na kukushukuru mapema kwamba utanipa kila hitaji langu katika wakati wako mtimilifu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon