Mambo ya Moyoni

Mambo ya Moyoni

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. —MITHALI 4:23

Mioyo yetu huwakilisha nia zetu na sehemu zetu za ndani kabisa. Ni muhimu kumhudumia Mungu kwa moyo safi. Mtu anaweza kufanya kitu kizuri, lakini asifanye kwa moyo mkamilifu. Mfalme Amazia alikuwa mtu kama huyo. Tunaambiwa kwamba alifanya mambo yaliyo ya adili lakini moyo wake haukuwa mkamilifu; na kwa hivyo Mungu hakupendezwa 2 Mambo ya Nyakati: 25:2).

Kuchukua muda ili kuchunguza nia zetu linaweza kuwa zoezi la uchungu, lakini linafaa. Kumhudumia Mungu kwa moyo wetu wote ndio hutuleta karibu naye.

Biblia inasema kwamba, hatufai kufanya mambo mazuri ili tuonekane na wanadamu, au kuomba ili kujipendekeza. Tukifanya tunayofanya kumpendeza Mungu, basi tuzo yetu itatoka kwake.

Chukua muda kwa maombi kutazama yote unayofanya na umwombe Mungu akufunulie iwapo nia zako zozote si safi. Iwapo si safi, basi unaweza kuzibadilisha kwa usaidizi wa Mungu. Fanya mambo unayoyafanya kwa sababu, kwa kweli unaamini kwamba ni mapenzi ya Mungu juu yako na uyafanye kwa utukufu wa Mungu. Ukifanya hivyo, undani na ukaribu wako na Mungu utaongezeka.

Mungu anajalishwa sana na kwa nini tunafanya mambo, kuliko ni mambo gani tunafanya. Watu huona matendo yetu lakini Mungu hutazama moyo!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon