Maombi Rahisi yaliyojaa Imani

Maombi Rahisi yaliyojaa Imani

Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. —YEREMIA 29:12

Wakati mwingine tunapoomba maombi rahisi, tukiwasilisha tu mahitaji au hitaji la mtu mwingine, tunafikiria kwamba tunafaa kufanya au kusema mengi zaidi. Lakini nimegundua kwamba nikiomba kile Roho Mtakatifu ameweka moyoni mwangu, bila kuongezea yaliyotokana na mwili wangu, maombi huwa rahisi sana na sio marefu.

Tunapochukua muda mfupi kumshukuru Mungu kwa kitu au kumwomba kitu, nia zetu hutuambia, “Sawa, hayo si marefu inavyostahili, au kwamba sio ya ufasaha inavyostahili. Unafaa kuomba kwa sauti na kwa nguvu iwapo unataka kwa kweli Mungu akusikie.”

Mara nyingi huwa tunafikira lazima tumpendeze Mungu au watu wengine na maombi yetu, hapo ndipo tunapokosa kufurahia burudani ambayo kila maombi rahisi ya imani yanafaa kuleta. Tunapoishi katika ushirika wa karibu na Mungu, tunaweza kusema kilicho moyoni mwetu na kuamini kwamba amesikia, na kwamba atakishughulikia kwa njia yake na kwa wakati wake.

Wakati wote watoto huwa mifano mizuri ya kufuata tunapotafuta ukawaida. Msikilize mtoto akiomba, na maisha yako ya maombi yatabadilika ghafla.


Acha maombi yawe ya kawaida na utayafurahia zaidi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon