Maombi ya Mtu Mwenye Haki

Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. —Yakobo 5:17

Yakobo anatuambia kuwa maombi ya bidii ya mtu “mwenye haki” yana nguvu (Yakobo 5:16). Huyu mtu ameweka imani yake ndani ya Yesu kwa wokovu na msamaha wa dhambi na hayuko chini ya hukumu—ni aliye na tumaini ndani ya Mungu na katika nguvu ya maombi. Haimaanishi mtu asiye na kasoro zozote katika maisha yake.

Eliya alikuwa mtu wa Mungu ambaye alikuwa akikosea wakati mwingine, lakini hakuruhusu makosa yake kuiba tumaini lake ndani ya Mungu. Eliya alikuwa na imani, lakini wakati mwingine tunaona hofu ndani ya maisha yake. Alikuwa mtiifu, lakini wakati mwingine, alikosa kuwa mtiifu. Alimpenda Mungu na kutaka kutimiza mapenzi yake na mwito wake juu ya maisha yake. Lakini wakati mwingine alikubali kushindwa na udhaifu wa wanadamu na kujaribu kuepuka matokeo.
Katika 1 Wafalme 18, tunamuona akitembea katika nguvu kuu, akiita moto kutoka mbinguni na kuwaua manabii 450 wa Baali. Halafu punde tu baada ya hapo, tunaona akitoroka kwa woga kutoka kwa Yezebeli, akiwa na fikra hasi na kufadhaika, na hata kutaka kufa.

Kama walivyo wengi wetu, Eliya anaacha hisia zake kumtawala wakati mwingine. Alikuwa mwanadamu tu kama sisi, ilhali aliomba maombi yenye nguvu. Mfano wake unafaa kutupatia “nguvu za kimaandiko” zinazotosha kushinda hukumu inapoinuka kutuambia kuwa hatuwezi kuomba kwa nguvu kwa sababu ya udhaifu na makosa yetu.


Usiwahi kupuuza nguvu za maombi yenye tumaini, matokeo, na bidii.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon