“Martha, Martha”

Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema,ambalo hataondolewa (LUKA 10:41-42)

Katika hadithi inayotuongoza  katika andiko la leo, Yesu alienda kutembelea akina dada wawili, Mariamu na Martha. Mariamu alijishughulisha kumwaandalia kila kitu- kusafisha nyumba, kupika, na kujaribu kufanya kitu kionekane tu kizuri machoni. Mariamu kwa upande ule mwingine, akachukua nafasi ya kuwa na ushirika na Yesu. Martha akamkasirikia dada yake, akitaka ainuke na kumsaidia na kazi. Hata akamlalamikia Yesu na kumwambia amwambie Mariamu ajishughulishe!

Jibu la Yesu lilianza na “Martha, Martha,” na hayo maneno mawili yanamaanisha zaidi ya vile huenda tukatambua. Yanatuambia Martha alikuwa na shughuli nyingi kiasi cha kukosa nafasi ya mahusiano, alikuwa anachagua kazi dhidi ya undani, na alikuwa anatumia muda wake vibaya na kukosa kilichokuwa muhimu.

Mariamu, hata ingawa alikuwa anatumika katika hekima; alikuwa anatumia wakati huo vizuri. Angalitumia muda wa maisha yake yote akisafisha lakini siku hiyo, Yesu alikuwa amekuja kwake, na alikuwa anataka ahisi kukaribishwa na upendo. Alikuwa amekuja kumwona yeye na Mariamu, sio kukagua nyumba yao safi. Huku nikifikiria kwamba nyumba safi ni muhimu, huu haukuwa wakati wa kuishughulikia. Ulikuwa wakati wa kumshughulikia Yesu kwa sababu alikuwa hapo.

Ninajikumbusha na kuwahimiza kutumia hekima na kutokosa uwepo wa Mungu ukiwepo. Kuna nyakati ambazo huwa tunahisi Roho Mtakatifu akituchochea kuomba au kukaa katika uwepo wake kwa maombi, lakini huwa tunachagua kufanya kazi au kucheza. Tunafaa kuitika mara moja anapoita. Baraka za uwepo wake zinapita manufaa ya kitu chochote ambacho tunaweza kufanya.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Usikose nafasi ya kufurahia uwepo wa Mungu.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon