Shukrani kwa Mchakato wa Mabadiliko

Shukrani kwa Mchakato wa Mabadiliko

Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho. 2 WAKORINTHO 3:18

Mabadiliko hayafanyiki ghafla, na mchakato huo unaweza kuonekana ni wa polepole wakati mwingine. Lakini hilo halibadilishi ukweli kwamba mojawapo ya faida za kuishi katika uhusiano na Yesu ni uhuru wa kusahau ya nyuma na kusonga mbele hadi kwenye kile Mungu alicho nacho kwa ajili yetu.

Unapojaribiwa kujihukumu kwa sababu ya maendeleo unayofikiria kwamba unafaa kuwa umefanya na hujafanya, rudisha macho yako kwa Yesu na ushukuru kwamba anafanya kazi yake timilifu katika maisha yako kwa wakati wake. Jikumbushe kwamba, “Mungu ananipenda na ana mpango mzuri juu ya maisha yangu. Bado sijafika, lakini niko sawa, na niko njiani!” Kumbuka kwamba kupitia kwa imani umefanywa mwenye haki kwa Mungu, na hata kama hujawasili kwenye utimilifu, unapiga hatua.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba unabadilisha maisha yangu katika wakati wako mtimilifu. Ninakuamini, na ninachagua kutohisi kuhukumiwa au kufadhaika tena. Uko kazini katika maisha yangu, na ninashukuru kwa sababu ya hilo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon