Kuwa na Mkabala wa Maisha Kama wa Mtoto

Kuwa na Mkabala wa Maisha Kama wa Mtoto

Basi yeyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. MATHAYO 18:4

Kitu kimoja tunachojua kuhusu watoto ni kwamba wao hufurahia maisha. Mtoto anaweza kufurahia kitu chochote. Mtoto anaweza kugeuza kazi ikawa mchezo ili aweze kuifurahia.

Ninakumbuka nikimwambia mwanangu wa kiume afagie varanda alipokuwa na umri wa miaka 11 au 12. Nilitazama nje na nikamwona akidensi na ufagio kwa muziki uliokuwa ukicheza katika kifaa cha muziki alichokuwa amevaa kichwani. Nikawaza, lo! Amegeuza kufagia kuwa mchezo. Iwapo atakuwa anafagia kila siku, atakuwa akifurahia kufanya hivyo.

Tunafaa kuwa na moyo kama huo sisi wote. Huenda tusichague kudensi na ufagio, lakini tuchague moyo wa shukrani katika vitu vyote tunavyofanya na kufurahia vipengele vyote vya maisha.


Sala ya Shukrani

Nikiwa katika hali ambayo kwa kawaida haionekani kufurahisha, Baba, nisaidie, kuifanya iwe ya kufurahia. Ninakushukuru kwamba ninaweza kufurahia kila sehemu ya maisha yangu, nikijua kwamba furaha ya Bwana ndiyo nguvu yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon