Mngoje Mungu

Mngoje Mungu

Maana mnahitaji subira, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. —Waebrania 10:36

Kuna wingi wa Wakristo ulimwenguni wasioridhika kwa sababu wanajaribu kufanya kitu fulani kifanyike, badala ya kungoja Mungu kwa uvumilivu ili atimize vitu kwa muda wake na kwa njia zake mwenyewe. Tuna haraka lakini Mungu hana.

Unyenyekevu unasema, “Mungu anajua vyema, na hatachelewa!” Kiburi kinasema, “Niko tayari sasa. Nitafanya vitu vifanyike kwa njia yangu mwenyewe.” Mtu mnyenyekevu hungoja kwa uvumilivu; kwa kweli ana “woga wa heshima” wa kufanya mambo kwa nguvu zake. Uvumilivu ni uwezo wa kuwa na fikra nzuri huku ukingoja. Lakini mtu mwenye kiburi hujaribu kitu kimoja baada ya kingine, bila mafanikio. Kiburi ni shina la kutovumilia.

Uvumilivu ni tunda la Roho Mtakatifu linalojidhihirisha katika fikra tulivu chanya bila kujali hali zetu za maisha. Usifikiri kuwa unaweza kutatua shida zako zote au kushinda matatizo peke yako. Tunaponyenyekea chini ya mkono mkuu wa Mungu, tunaanza kufa kwa njia zetu na nyakati zetu na kuwa na uamsho kwa mapenzi na njia za Mungu kwetu sisi.


Ni kupitia tu kwa subira na uvumilivu katika imani ambapo tunapokea ahadi za Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon