Moto wa Hata Dhamira Kuu Zaidi

Moto wa Hata Dhamira Kuu Zaidi

Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena. MITHALI 24:16

Watu wanapojaribu kitu, lakini wasifanikiwe, mojawapo ya sababu za kimsingi ambazo huwafanya wakate tamaa ni kwamba wanahisi kama “mshindwa.” Ukweli ni kwamba huwa hatuwi washindwa hadi tukate tamaa. Hata ingawa tunajaribu tuwezavyo, sisi wote tuna wakati ambao vitu havifanyiki vile tulivyokuwa tumetarajia vitafanyika. Tunaweza kushindwa kwa kitu kimoja, au hata vitu vichache, lakini hilo bila shaka halitufanyi kuwa washindwa maishani.

Amini usiamini, tunafaa kushukuru kwa ushinde tunaokumbana nao kwa sababu unasaidia kututayarisha kwa mafanikio yajayo. Kushindwa katika mambo mengine hutunyenyekeza na kutufundisha mambo tunayohitaji kujifunza kwa ajili ya changamoto iliyo mbele yetu. Hufai kuhisi kushindwa kutokana na ushinde; ona ushinde kama moto wa dhamira kuu na mafaniko ya siku zijazo.


Sala ya Shukrani

Baba, nikiwa katika hali ngumu na kujaribiwa kukata tamaa, nisaidie kukumbuka kwamba uko nami. Asante kwamba unanipa nguvu na dhamira ya kuendelea. Na asante kwamba bila kujali linalofanyika, ninajua una mpango mwema juu ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon