Moyo wa Utambuzi

Moyo wa Utambuzi

Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe, katika njia zako zote mkiri yeye naye atayanyosha mapito yako. —MITHALI 3:5– 6

Watu wanaoelekea kufikiria kuhusu vitu kupita mipaka huwa wana wakati mgumu na imani. Tukifikiria kitu kupita mipaka, kuwa na wasiwasi na kujawa na fikra kuhusu vile tunavyoweza kutatua tatizo fulani au kutengeneza nafasi fulani, tutakuwa mara nyingi tunajiamini badala ya kumwamini Mungu.

Nilikuwa mwazaji wa kupita mipaka wa kiwango cha A. Nilikuwa ninalazimika kufikiria kiutaratibu vile mambo yatakavyokuwa. Nilikuwa tayari nina mpango ambao nilikuwa nao na nilikuwa nikiufurahia. Nilikuwa nikijiuliza bila kikomo, “Kwa nini, Mungu? Lini, Mungu, Lini?” Kisha siku moja Bwana aliunenea moyo wangu na kusema, “Mradi tu unatumia nia yako kimantiki hutawahi kuwa na utambuzi.”

Utambuzi huanzia moyoni na kwenda juu kutia nuru nia. Mradi tu nia yangu ilikuwa ikijishughulisha kuwaza bila kuhusisha Roho Mtakatifu na kinyume na ukweli ulio ndani ya Neno la Mungu, Yesu hangenifikia. Anataka tutumie nia zetu kimantiki, lakini anataka tufikiria kimantiki kwa njia ambayo inawiana na Neno lake na kumruhusu kuwa katika udhibiti.

Nimegundua kwamba ninaweza kufikiria kimantiki kuhusu suala fulani hadi lianze kunichanganya, na hilo linapofanyika, ni ishara kwangu ya kuliachilia na kuacha Mungu anifunulie kile tu anaweza kunionyesha.


Tukijaribu kufikiria kwa nini kila kitu kinafanyika maishani, hatutakuwa na amani ya nia wala moyo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon