Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo… (MALAKI 3:2)
Mungu hutumia moto wake usafishao kutubadilisha na kutufanya watu anaotaka tuwe. Nimegundua kwamba si rahisi kubadilika. Nimekuwa nikisoma Neno la Mungu kwa miaka thelathini, na bado lazima nifanye vitu vingi na kumruhusu Mungu kunibadilisha kwa njia fulani. Ningali sijafika ninapohitajika kuwa, lakini ninashukuru Mungu kwamba siko nilipokuwa.
Tukiwa wasumbufu au kukosa hiari ya kutubu, moto usafishao wa Mungu unapokuja kufunua tabia fulani inayohitaji kubadilishwa ndani yetu, basi upendo huwa msumbufu. Acha nieleze. Tunajua kwamba Mungu ni upendo, na ni mwenye wivu. Hataki kitu chochote ndani yetu kichukue nafasi yake. Na upendo, Mungu mwenyewe, atakuwa na wivu na msumbufu bila kuchoka hadi anapopenya katika maisha yetu. Upendo (Mungu) utatuonyesha vitu tusivyotaka kuona ili utusaidie kuwa tunachohitaji kuwa.
Moto hula uchafu wote na kuacha vyote ambavyo vimebaki vikiwa vimewaka kwa sababu ya utukufu wa Mungu. Wingi wa Joyce Meyer wa kale amechomwa katika moto usafishao wa Mungu kwa kipindi cha miaka mingi. Bila shaka haijakuwa rahisi, lakini imekuwa ya kufaa.
Huenda moto wa Mungu usafishao ukakujilia kwa njia nyingi tofauti. Huenda ukawa na mguso moyoni mwako wa kuacha kufanya kitu na kuanza kufanya kingine; unaweza kuhisi uthibitisho anapoanza kuzungumza nawe kupitia kwa Neno lake; au huenda ukasikia moja kwa moja kutoka kwa Roho wake hadi kwa roho yako. Vyovyote vile inavyokuja, Mungu ataleta moto wake usafishao katika maisha yako. Unapokuja, usiupinge, lakini amini Mungu na uache moto ufanye kazi.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO:
Mungu anakubadilisha kila siku na leo uko bora kuliko vile ulivyokuwa jana.