Mungu ataongoza safari yako

Mungu ataongoza safari yako

Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake.  —Zaburi 37:23

Maisha ya Kikristo yanaweza kulinganishwa na safari. Roho Mtakatifu ndiye kiongozi wetu … Anatuongoza kila siku. Na Yeye daima anatuongoza katika kile kinachofaa kwa maisha yetu. Funguo la safari ya mafanikio na ya kufurahisha ni kumfuata.

Lakini kumfuata Mungu kunamaanisha nini? Kimsingi, inamaanisha kumtii, kufuata uongozi wake, na kufanya kile anachosema Mara nyingi tunakimbia mbele ya Mungu. Tunaweza kufikiria tunajua mwelekeo bora wa kuchukua au tunakosa uvumilivu kwa muda wake na kuchukua hatua mbaya kwa vile inakaa ya haraka.

Tatizo ni, tukigundua kuwa barabara hiyo inaongoza kwenye mwisho wa wafu, tutapaswa kurudi tena mahali ambapo tuliondoka kwenye njia mwafaka.

Habari njema ni, Mungu yuko pale, akisubiri kutuongoza tena na kutuonyesha njia sahihi ya kwenda.

Bwana amepanga vizuri safari ya kila mmoja. Tunahitaji kuelewa kikamilifu kwamba anatupenda, kwamba ni mwema na mwenye haki na tunaweza kumwamini Tunaweza kumtegemea Yeye kutuongoza katika mwelekeo unaofaa kwetu. Tunaweza kumtegemea Yeye kutusahihisha tunapopotea na kutuongoza kwenye mahali pa haki. Tunaweza kumwamini yeye na wengine juu ya njia yetu. Tunaweza kumwamini Yeye kwa maisha yetu … tosha!

Fuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, kwa sababu Yeye anajua njia na atakuwa daima na wewe. Mwamini Yeye kukuongoza katika mema yote aliyopanga kwa ajili yako muda mrefu kabla hujazaliwa. Na ufurahie safari.


Ombi La Kuanza Siku

Mungu, Neno lako linasema kwamba Wewe huelekeza hatua za waumini. Ninaamini wewe unaniongoza kwenye safari uliyonayo kwa ajili yangu, na najua kwamba nitakapotoka kwenye njia, utakuwa daima nami kunisaidia kurudi  na kuendelea.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon