Mungu Hachelewi

Mungu Hachelewi

Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. —WAGALATIA 6:9

Watu wengi hufikiri kwamba ni wavumilivu ati kwa sababu wamelazimika kungoja kitu. Lakini uvumilivu ni zaidi ya kungoja. Uvumilivu ni kuwa na nia njema, yenye matarajio na furaha katika mchakato wa kungoja. Ni tunda la Roho ambalo hujidhihirisha ndani ya aaminiye ambaye amejitwaa kwa Mungu, bila kujali hali yake. Mtu mvumilivu huwa mtulivu na kutuelekeza kwa upaji wa Baba yetu wa mbinguni.

Mara nyingi huwa tunataka mpango wa Mungu juu ya maisha yetu ufanyike sasa hivi. Lakini kazi ya Mungu timilifu huchukua muda na utuhitaji kuwa wavumilivu. Mungu hafanyi kazi kwa ratiba yetu. Ingawa tuna haraka na wasiwasi, Mungu hana hayo. Huchukua muda kufanya mambo vizuri—Huitengeneza kazi yake kwa uangalifu, kwa fikra na utaratibu.

Sisi ni kazi ya Mungu (Waefeso 2:20). Yeye ni msanifu, na anasanifu kwa ustadi kitu kizuri kutokana na maisha yako. Wakati wa Mungu unaonekana kuwa siri yake ndogo. Biblia inatuahidi kwamba hatawahi kuchelewa, lakini pia nimegundua kwamba mara nyingi haji mapema. Hata ufanye nini, huwezi kumharakisha Mungu. Kwa hivyo ninakuhimiza kufurahia kungoja.


Furahia ulipo unapokuwa njiani kuelekea unakokwenda!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon