Mungu Hatawahi Kukuacha

Mungu Hatawahi Kukuacha

. . .Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu. YEREMIA 31:3

Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya vile maisha yako yalivyo na vile unavyofikiria kujihusu. Tunahitaji kujifunza kuwaza vile Mungu anavyowaza. Lazima tujifunze kujitambulisha na Kristo na mtu mpya ambaye ametuumba kuwa.

Katika Andiko, Mungu anatumia maneno kama vile “rembo,” “stahili,” “thaminiwa,” na “ghali” anapoongea juu ya wanawe. Hakuna shaka kwamba tumepungukiwa na utimilifu, kwamba tuna kasoro na udhaifu, lakini Mungu ni Mungu na hutuona vile anajua tunaweza kuwa.

Hutuona kama mradi uliokamilika huku tukiendelea na safari. Huona mwisho kutoka mwanzo na hajali kinachotokea hapo katikati. Hapendezwi na dhambi zetu na tabia mbaya, lakini hatawahi kutuacha na hutuhimiza kuchuchumilia mbele wakati wote. Mungu anakuamini!


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba wewe ni Baba mwema ambaye ananipenda bila masharti. Niasidie kujiona vile unavyoniona. Asante kwamba hata kama mimi ni kazi inayoendelea, tayari una matokeo yaliyokamilika katika nia yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon