Mungu Huchagua Wasiofaa

Mungu Huchagua Wasiofaa

Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu. —1 WAKORINTHO 1:27

Unapohisi kukata tamaa, kumbuka kwamba Mungu alikuchagua kwa kusudi lake, hata kama hujihisi kwamba wewe ni mtahiniwa anayestahili. Kwa kufanya hivyo, ameweka mbele yako mlango uliyo wazi ili kukuonyesha neema, rehema na nguvu zisizo na mipaka ili abadilishe maisha yako.

Mungu anapotumia mmoja wetu, hata ingawa sisi sote tunaweza kuhisi kwamba hatutoshi na hatufai, tunatambua kuwa chanzo chetu hakipo ndani yetu lakini ndani yake peke yake: “Hili ni kwa sababu kitu kipumbavu ambacho kina chanzo ndani ya Mungu kina hekima kuliko wanadamu, na kitu dhaifu kinachotokana na Mungu kina nguvu kuliko wanadamu” (1 Wakorintho 1:25).

Kila mmoja wetu ana kusudi, na hatuna kisingizio cha kukosa kulitimiza. Hatuwezi kutumia udhaifu wetu kama kisingizio kwa sababu Mungu anasema kwamba nguvu zake hutimilika katika udhaifu (2 Wakorintho 12:9). Hatuwezi kutumia mambo yaliyopita kama kisingizio, kwa sababu Mungu anatuambia kupitia kwa Mtume Paulo kwamba mtu yeyote akiwa ndani ya Kristo, ni kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! yamekuwa mapya (2 Wakorintho 5:17).

Chukua muda peke yako na ufanye hesabu kuhusu jinsi unavyojihisi. Picha yako kujihusu ni ipi? Unajiona ukiwa umeumbwa tena katika mfano wa Mungu, umefufuliwa kwa maisha mapya kabisa ambayo yanakungoja uyadai?


Kila mmoja wetu anaweza kushinda katika kuwa kila kitu ambacho Mungu alikusudia awe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon