Mungu Huwa Nasi Wakati Wote

Kwa maana ndivyo alivyo Mungu, Mungu wetu. Milele na milele yeye ndiye atakayetuongoza. (PSALM 48:14)

Ni jambo la kutuliza kuamini kwamba Mungu ameahidi kutuelekeza tunapokuwa katika dunia hii. Hatuko pekee yetu, kwa kuwa yuko nasi kila wakati. Hutuangalia kila wakati.

Unapoanzisha uwezo wako wa “kusikia” kutoka kwa Mungu, lazima ukumbuke kwamba mwelekeo wa kiungu ni mojawapo wa njia kuu anazotumia kuzungumza. Fanya tabia ya kiroho ya kumtambua Mungu katika kila unalofanya, ukimwomba mwelekeo wake halafu kuamini kuwa unao.

Nitaenda kununua vitu baadaye leo na nitamwomba Mungu aniongoze. Huenda akaniongoza kwenye mnada ambao sikutarajia, au nikiwa huko nje, huenda akanielekeza kwa njia ya mtu ambaye anahitaji himizo. Ninaamini kwamba hatua zangu huongozwa na Bwana (soma Zaburi 37:23). Ninaamini Mungu kuniongoza kwa kile ninachotaka kununua na kunisaidia kutokununua vitu nisivyohitaji. Ninataka ahusike katika kila kitu ninachofanya na ninafikiri ni vivyo hivyo nawe pia.

Katika huduma yangu ya ufundishaji, wakati wote huwa nina uzoefu wa kupata mwelekeo wa kiungu. Ninasoma na kuandaa ninachoamini nitazungumza, lakini kila mara ninapoanza kuzungumza, ninajipata nikiwa ninaongozwa na Mungu upande tofauti na ule nilikuwa nimepanga. Anajua kile ambacho watu waliohudhuria wanafaa kusikia na ni kazi yangu kumruhusu kuchukua uongozi.

Ninakuhimiza kukumbuka kwamba kusikia kutoka kwa Mungu mara nyingi huonekana kuwa jambo la kawaida kabisa. Usitafute tajriba za kiungu, lakini badala yake, tafuta uelekezi wa kiungu. Roho wake yuko ndani yako na hufurahia kuhusika katika shughuli zako zote. Chochote unachofanya leo au mahali popote utakapoenda, mtarajie kukuongoza.

NENO LA BWANA KWAKO LEO:

Mungu yuko nawe kila wakati na atakuelekeza katika kila kitu unachofanya leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon