Mwenye Nguvu na Nguvu Ndani ya Bwana

Mwenye Nguvu na Nguvu Ndani ya Bwana

. . . Nitakutia nguvu, naam nitakusaidia , naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. ISAYA 41:10

Fikiria maisha yako. Je, kuna hali ambazo unashughulikia vizuri sasa hivi ambazo awali zingekufanya uhisi hofu na mfadhaiko? Bila shaka zipo. Vile umekuwa ukitembea na Mungu amekuwa akikutia nguvu na kukufanya uwe na roho ngumu kwa matatizo—unaweza kushukuru kwamba una nguvu zaidi kuliko vile ulivyokuwa.

Katika njia hiyohiyo, ninaweza kukuhakikishia na kukuhimiza kwamba baadhi ya vitu vingine vinavyokusumbua sasa hivi havitakuathiri kwa njia hiyo moja katika miaka mitano ijayo. Mara nyingi tunapofanya vitu kwa mara ya kwanza, huwa tunang’ang’ana, lakini baada ya kupata tajriba kiasi, huko kung’ang’ana kunaisha. Tunaweza kuchuchumilia kupita kwenye vizuizi na kukosa kuruhusu hali kutudhibiti. Badala yake, amini Mungu na ujue kwamba anafanya kazi katika maisha yako katika kila hali.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kujifunza kutoka kwako katika kila hali ninayokabiliana nayo. Ninakushukuru kwamba nina nguvu kuliko vile nilivyokuwa, na ninakushukuru kwamba unanitia hata nguvu zaidi kupitia kwa hali zangu za sasa. Ninaweka imani yangu ndani yako, nikijua kwamba hakuna kilicho kigumu kwako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon