Nanga ya matumaini

Nanga ya matumaini

Tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, Waebrania 6:19

Sisi sote tunapitia wakati mgumu katika maisha yetu, na kama meli katika dhoruba, tunahitaji msaada wa kubaki thabiti. Meli ina nanga ili kusalia imara, na Biblia inasema kuwa nanga ya nafsi yetu ni matumaini.

Wakati wewe na mimi tunathamini tumaini letu kwa Mungu na Neno Lake, tunaweza kuhisi dhoruba na mawimbi, lakini mwisho hatutahamishwa.

Wakati wa dhoruba, tumaini linatupa uwezo wa kuangalia mambo kama yalivyo na bado tuna hakika kuwa kitu kizuri kinakuja. Hiyo inafanya tumaini kuwa kitu bora sana na muhimu kwa wewe na mimi kuwa nacho na hasa-wakati wa shida. Kwa kweli, naamini huo ndio msingi ambao imani yetu inapaswa kujengwa.

Hakuna mtu-hata Mungu-anaweza kuahidi kwamba hatuwezi kamwe kukabiliana na kukatishwa tamaa au taabu. Lakini jambo muhimu ni kwamba hatuwezi kuacha tumaini. Kudumisha mtazamo mzuri na kuzingatia matumaini tuliyo nayo katika Kristo inatuweka katika nafasi ya kuona nguvu ya Mungu ya miujiza.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, ninaweka tumaini langu ndani yako. Imani yangu ndani yako na matarajio ya mambo makuu Unayoyafanya katika maisha yangu ni nanga yangu katika nyakati za majaribu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon