Neno la Hekima

Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima (1 Wakorintho 12:8)

Wakorintho wa kwanza 1:30 inasema kwamba Yesu “amefanywa kwetu hekima” itakayo kwa Mungu. Na mwandishi wa kitabu cha Mithali anarudia mara nyingi kutuambia tutafute hekima na tufanye tuwezavyo kuipata. Hekima inaweza kupatikana na watu wote, lakini “neno la hekima” ni aina ya hekima iliyo tofauti na ambayo kile mtu anaweza kuwa nayo.

Hekima yote hutoka kwa Mungu, na hekima unayoweza kujifunza kutokana na tajriba na kupatikana kiakili. Hilo silo neno la hekima lililotajwa katika andiko la leo. Neno la hekima ni aina ya uelekezi wa kiroho. Linapotumikishwa, mtu hufanywa kujua kimiujiza kwa Roho Mtakatifu jinsi ya kushughulikia jambo fulani kwa njia ya kipekee yenye hekima, ambayo inazidi masomo au tajriba ya kawaida na ambayo inakubaliana na kusudi la Mungu.

Huwa tunatumika katika karama hii hata bila kujua. Huenda tukamwambia mtu kitu ambacho kinaonekana kuwa cha kawaida kwetu lakini kwa msikilizaji, ni neno la hekima kwa ajili ya hali yake.

Nimepokea maneno ya hekima kutoka kwa watoto ambao kwa hakika nilijua hawakujua walichokuwa wanasema. Roho Mtakatifu alikuwa anataka nimsikilize na alitumia chanzo ambacho ningejua kwamba ni yeye aliyekuwa akizungumza. Mwombe na kutarajia uelekezi wa Mungu kupitia kwa maneno ya hekima.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Tafuta hekima kwa sababu neno moja la hekima linalozungumzwa kwa wakati unaofaa linaweza kuwa la kubadilisha maisha.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon