Nguvu ya Moyo Uliogeuzwa

. . . Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo. —1 SAMWELI 16:7

Mungu ni Mungu wa mioyo. Haangalii tu sura ya nje ya mtu, au vitu ambavyo mtu hufanya, na kuhukumu mtu kwa kigezo hicho. Mtu huhukumu mwili, lakini Mungu huhukumu moyo.

Inawezekana kutenda matendo mazuri na bado uwe na nia isiyo sawa. Inawezekana pia bado kufanya na mambo mengine vibaya lakini bado uwe na nia nzuri ndani. Mungu huelekea kutumia mtu aliye na nia nzuri na mwenye makosa kuliko kutumia mtu ambayo huonekana kuwa mzuri, anayestahili kwa sura yake ya nje lakini aliye na moyo mwovu.

Ni muhimu kuyajua maisha yetu ya ndani na nia za mioyo yetu, vile tunavyohisi na kufikiria kuhusu vitu (Kile Biblia inaita mtu wa moyo aliyejificha), iwapo tunataka kusikia kutoka kwa Mungu na kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu.


Mungu anapotafuta kumwinua mtu, huchagua mtu aupendazaye moyo wake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon