Nguvu za Kutenda Mema

Nguvu za Kutenda Mema

. . . Jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye huko na huko , akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye. MATENDO YA MITUME 10:38 BIBLIA

Ninaamini bila shaka yoyote kwamba tunapokuwa na shida, hatufai kuwa na wasiwasi, lakini tnahitaji pia kuendelea kufanya vitu tunavyojua kufanya. Kwa mfano, ukiwa na wajibu wa kufanya, hakikisha umefanya. Mara nyingi, watu wanapopitia katika shida za kibinafsi, wanajitenga kutoka kwa maisha ya kawaida na kutumia muda wao mwingi wakijaribu kusuluhisha shida hiyo. Kitendo hiki kisichozalisha chochote huwazuia kufanya wanachopaswa kuwa wakifanya, ambacho ni “kutenda mema.”

Zaburi 37:3 inasema kwamba tunafaa kumwamini Bwana na kutenda mema na tutakula kwa uaminifu wake. Uaminifu wa Mungu ni kitu ambacho sisi wote tunaweza kushukuru kwacho! Nimegundua kwamba nikiendelea kusoma Neno la Mungu, kuendelea kuomba, kutenda wajibu wangu, na kusaidia watu wengi zaidi niwezavyo, ndipo ninapata upenyo haraka zaidi. Kusaidia watu wengine huku tukiwa bado tumedhurika mioyo ni kitu cha nguvu sana.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba sitawaliwi na shida zangu. Ninapopitia katika shida, ninaweza kusaidia walio karibu nami. Ninashukuru kuwa kwa usaidizi wako, ninaweza kuwatendea wengine mema; ninaweza kuleta utofauti ulimwenguni.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon