Nitabadilika Vipi?

Nitabadilika Vipi?

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. —Warumi 12:2

Mabadiliko hayaji kwa kung’ang’ana, bidii za mwanadamu bila Mungu, masikitiko, kujichukia, kujikataa, hukumu, wasiwasi au kazi za mwili. Sisi ni viumbe vipya ndani ya Yesu (2 Wakorintho 5:17), na kwa sababu ya hiyo sisi sote tunataka kumpendeza Mungu. Tunataka kuwa anachotaka tuwe, na kufanya vile anavyotaka tufanye, lakini ili hilo lifanyike, tunahitaji kujifunza kufikiri vile anavyofikiri.

Mabadiliko katika maisha yako huja kwa kugeuza nia yako kwa Neno la Mungu. Unapokubaliana na Mungu na kuamini kwa kweli kwamba anachosema ni kweli, polepole inaanza kudhihirika ndani yako. Unaanza kuwa na fikra tofauti, halafu unaanza kwa kuzungumza kwa utofauti na mwishowe unaanza kufanya mambo kwa utofauti. Huu ni mchakato unaendelea kwa hatua, lakini unapoendelea kufanyika, bado unaweza kuwa na fikra kwamba, “Niko sawa, na niko njiani!”

Furahia unapobadilika. Furahia mahali ulipo unapokuwa njiani kuelekea unakoenda. Furahia safari! Usiharibu wakati wako wa “sasa” ukijaribu kukimbia kuelekea katika siku zijazo. Tulia. Acha Mungu awe Mungu. Acha kujikulia mgumu. Mabadiliko huja polepole, lakini katika mchakato huo, unamkaribia kila siku.


Tunaweza kuja kwa Yesu vile tu tulivyo. Anatuchukua tulivyo na kutufanya tunachostahili kuwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon