Njia Nzuri Kabisa ya Kuishi

Njia Nzuri Kabisa ya Kuishi

Hawa wanataja magari na hawa farasi, bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. ZABURI 20:7

Tunaweza kuishi kwa kujaribu kujishughulikia au tunaweza kuishi kwa kumwamini Mungu. Kumwamini Mungu ndiyo njia nzuri na ya amani kabisa ya kuishi, na, shukuru kwamba ni uamuzi tunaoweza kufanya kila siku.

Iwapo uko chini ya mshinikizo kwa sababu unajaribu kujishughulikia, basi amua kukoma wewe mwenyewe kujaribu kufanya kila kitu kifanyike, katika wakati wako, kwa njia yako, kulingana na mpango wako. Badala yake, mwegemee Mungu katika kila hali na uombe: Bwana, chochote kile ninachotamani katika maisha, iwapo hutaki niwe nach, sikitaki. Iwapo unataka niwe nacho, ninakuomba na kuamini kuwa utanipa kwa wakati wako, kwa njia yako, kulingana na mpango wako wa uungu.

Ukijiachilia kwa Mungu katika njia hii, utaona vitu vya ajabu vikifanyika katika maisha yako.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba ninaweza kufurahia amani yako huku ukiniongoza na kutenda mapenzi yako katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon