Nyakati za Tatizo

Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. —MATENDO YA MITUME 2:21

Miaka mingi iliyopita, kabla ya sheria ya mikanda ya usalama, rafiki yangu alikuwa akiendesha gari akiwa na mwanawe wa kiume mdogo akipitia kwenye barabara panda siku moja. Mlango wa upande wa abiria wa gari, haukuwa umefungika vizuri, na akageuka vikali. Mlango wa gari ukafunguka, na mwanawe akabingiria mpaka nje kwenye msongamano wa magari! Kitu cha mwisho ambacho rafiki yangu aliona ilikuwa seti ya magurudumu ya gari yakiwa karibu kumpanda mwanawe. Alichojua kufanya ni kulia, “Yesu!”

Alisimamisha gari lake na kumkimbilia mwanawe. Kwa mshangao wake, mwanawe alikuwa salama kitimilifu. Lakini mwanamume aliyekuwa anaendesha gari ambalo nusura limgonge mwanawe alikuwa na jazba.

“Usifadhaike!” Mwanangu yuko salama. “Shukuru Mungu uliweza kusimama!”

“Huelewi!” huyo mwanamume akajibu. “Sikugusa breki zangu!”

Hata ingawa hakuna kitu ambacho huyo mwanamume angefanya, jina la Yesu lilishinda na maisha ya mtoto huyo yakaokolewa.

Katika nyakati za matatizo, liite jina la Yesu. Kadri mimi na wewe tunavyoona alivyo mwaminifu wakati wa hitaji na tatizo—ndivyo tutakavyoshuhudia uweza wa nguvu za jina lake juu ya hali na mazingira—kadri imani yetu inavyozidi kukua, ndivyo tumaini letu linavyokua, na ndivyo tutamkaribia hata zaidi.


Kuna nguvu katika jina la Yesu kwa kila tatizo ambalo utawahi kukabiliana nalo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon